Kwa mujibu wa shirika la habari la ABNA, Axios ikinukuu afisa wa Marekani ilidai kwamba Iran na Marekani zimefikia makubaliano ya kusitisha mashambulizi ya pande zote na kufanya mkutano wiki hii.
Kwa mujibu wa madai ya afisa huyu wa Marekani, Iran na Marekani zitafanya mkutano Jumanne ijayo katika mji wa Doha kwa ajili ya kusuluhisha tofauti zinazohusiana na Mlango wa Hormuz.
Kabla ya hapo, gazeti la The New York Times likinukuu afisa mkuu wa Marekani lilidai kwamba mazungumzo ya kiufundi na Iran kuhusu namna ya kutekeleza mkataba, bado yamepangwa kwa siku zijazo.
Afisa huyu wa Marekani akirejelea makabiliano ya hivi karibuni kwa risasi kati ya Iran na Marekani alidai kwamba hakuna mazungumzo yaliyoghairiwa na mawasiliano bado yanaendelea.
Hii inatokea wakati ambapo masaa machache kabla gazeti la The Wall Street Journal lilikuwa limedai kughairiwa kwa mazungumzo ya wiki hii nchini Uswisi.
Your Comment